Enock Bella Amefunguka Kuhusu Kuvunjika Kwa Yamoto Band

Msanii kutoka katika kundi lililovunjika la Yamoto Band amefunguka na kudai kuwa mashabiki wao wasitegemee kuwaona wanakundi hao wanafanya kazi pamoja muda wowote kuanzia sasa.

Enock Bella alipokuwa anafanya mahojiano na kituo cha televisheni cha East Africa amefunguka kuwa pamoja na watu wengi kudai kuwa bendi hiyo imekufa lakini yeye hana taarifa hizo bali anachojua kuwa wamepeana nafasi ili kila msanii aweze kufanya kazi kivyake kwanza ila endapo kama kuna siku akiitwa au wakihitajika kupiga shoo kwa pamoja basi hatakuwa na neno bali ni kwenda na kushiriki na wenziye.

Enock Bella ambaye kwa sasa anafanya muziki wake kama msanii wa kujitegemea ameweka wazi kuwa kwa sasa kundi hilo kurudi kama zamani itakuwa ngumu ila kama ikitokeaa kufanya kazi ya mara moja basi watafanya makubaliano fulani ila kwa sasa kila msanii anafanya vizuri mwenyewe;

Sifikirii kwa sasa hivi labda kwa baadae ila kwa sasa kuiona Yamoto Band kama zamani kwa muda huu ambao tunao kwa sasa kusema kweli nitadanganya ila kwa baadae kinaweza kutokea chochote kile ila sio kwa sasa ila baadae naomba tuamini kuwa inaweza ikawezekana”.
Enock Bella ambaye ametoa wimb wake wa kwanza tangu ahame ya Yamoto ameonekana yupo mbali kidogo kulinganisha na wenzake kama Aslay ambaye anafanya vizuri na ametoa jumla ya nyimbo kumi na tatu tangu ahame bendi hiyo, pia wasanii wengine wanaofanya vizuri ni Becka Flavour ambaye anazidi kukimbiza katika jukwaa la Fiesta.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*