Kijana Huyu ndiye binadamu wa kwanza duniani mwenye uwezo wa kuzungusha kichwa hadi nyuzi 180 (+video)

Katika maisha kuna mambo mengi tutaendelea kuyaona hii ni kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na muingiliano wa vitu kibao vinavyosababisha genes za binadamu kubadilika kila uchao.

Huko nchini Pakistani amepatikana kijana mwenye uwezo wa kuzunguusha kichwa chake kuanzia mbele hadi nyuma yaani kwa nyuzi mlala wa 180.

Kijana huyo aliyetambulika kwa jina la Muhammad Sameer (14) mzaliwa wa mjini Karachi amezua gumzo nchini humo baada ya video yake kusambaa mitandaoni ikimuonesha akizunguusha kichwa chake mithili ya ndege bundi.

Kijana huyo akielezea jinsi alivyoanza mazoezi hayo hadi kufikia hatua hiyo, Sameer amesema kuwa kipindi akiwa na miaka 6 aliona muigizaji kwenye filamu moja ya kihindi akifanya hivyo ndipo alipoamua kuanza mazoezi ya kujifunza jinsi ya kugeuza kichwa.

“Nilianza taratibu kujifunza kugeuza shingo yangu baada ya kuona muigizaji mmoja kwenye filamu ya kuogopesha akizunguusha kichwa chake hadi mgongoni, nilistaajabu sana kuanzia hapo nikaanza kujifunza taratibu ingawaje mama alinipiga sana akinikataza kufanya hivyo ila sikukata tamaa kwa vile nilijua nina kipaji.“amesema Sameer kwenye mahojiano yake na Daily Mail.

Hata hivyo, Sameer amelazimika kuacha masomo yake ya elimu ya msingi na kujiunga na kikundi cha watumbuizaji maarufu mjini Karachi kijulikanacho kwa jina la ‘Dangerous Boys’ ili kuisaidia familia yake kifedha.

“Baba yake na Sameer (Sajid Khan, 49) alipata matatizo ya moyo mara mbili hivyo akaacha kazi kwa sasa yupo nyumbani. Hivyoikaniwia vigumu kumsomesha sikuwa na uwezo lakini Mungu ni mwema kwa sasa tunamtegemea yeye kwani kila siku hutuletea Rupia 500 (tsh elfu 13) ambazo zinatusaidia kuendesha familia.“amesema mama mzazi wa Sameer aitwaye, Rukhsana Khan.

Kijana huyo Sameer na wenzake wanane wanaounda kundi la ‘Dangerous Boys’ wanatumbuiza jijini Karachi kwenye kumbi za Starehe na huingiza kiasi cha Euro 6 hadi 8 kwa siku.

Hata hivyo, huenda akawa ndio binadamu wa kwanza kufanya hivyo duniani kwani mpaka sasa hakuna binadamu aliyeripotiwa kuwa na uwezo huo.

Tazama picha na video za kijana huyo akifanya maajabu hayo hapa chini (Video & Picha by Daily Mail)

 

 

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*