Usitumie Vigezo hivi Kuharakisha Ndoa

Watu wengi hasa vijana wamekuwa na tabia ya kufunga ndoa za haraka haraka na wapenzi wao kwa sbabu tu kuna vitu wanhisi vitakaa sawa katika maisha.ndoa ni jambo la kheri lakini inapaswa kuwa la amani na utulivu kwa sababu yule unaenda kuisi nae itatakiwa kuishi nae maishayako yote, muda ambao hauwezi kuhesabu maana haujui ni lini mmja wenu atatangulia. zifuatazo ni sababu za kuepuka kufunga ndoa kwa haraka.

1.Umri wangu umekwenda sana

Hii inawakumba sana wanawake wengi husema kuwa wanazeeka hivyo ujikuta wakipanga kabisa kuwa ikifika umri fulani ni lazima niwe nishaolewa na nina watoto kadhaa,kulingana na unyeti wa swala la ndoa watu hawapaswi kukimbizana na muda bali kusubiri muda ukifika na kuingia kwenye ndoa ili isikuletee matatizo.

2.Kigezo cha mali na utajiri wa mwenzi wako.

Kuna baadhi ya wati wanajikuta wanaingia katika mahusiano na kutaka kuoa au kulewa na watu waliowazidi kipato kwa sababu tu anaamini kuwa mtu huyo ataweza kuyaendesha maisha yake kwa sababu ya ela,huko ni kijidanganya, ndoa inahitaji mapenzi na maelewano usije ukaingia na mtu mwenye kuzidi uwezo ukawa mtumwa.

3.Kujifananisha na watu wako wa karibu(marafiki)

Wapo watu wanendeshwa sana na maisha ya watu wa pembeni, kuna baadhi wanaumia roho kuwa kwanini rafiki yangu kafanya hiki na mimi sijafanya, kwanini fulani kaoa au kaolewa mimi bado , hivyo anajikuta kulazimisha ndoa ambayo bado au mtu ambae sio sahihi kwa sababu tu rafiki zake wameoa na kuolewa.

4.Kuwa karibu na yule umpendae.

Inawezekana labda kwa sababu ya umbali ndo maana labda kunakuwa na mikwaruzano ya hapa na pale lakini hii isiwafanye wawili wakaazimisha kufunga ndoa wakitegemea itakuwa njia bora ya kuimarisha mahusianao na kuwa karibu zaidi.

5,Niondoke katika nyumba ya familia

Wapo wanaokuwa wanahisi kuchoka kukaa nyumbani, anahisi kubanwa na ndugu zake na mambo kama hayo, hivyo anapopata mwanaume wa kuwa nae katika mahusiano anataka kufanya ndoa ya haraka itakayo mfanya atoke nyumbani.Hili sio jambo jema kabisa maana haujui unakoenda unaenda kukimbilia nini kikubwa au kidogo zaidi.

6.Kisasi kwa uliyekuwa nae nyuma

Usifanye kitu kwa ajili ya kumkomesha mwingine, wapo watu wanafunga ndoa ili tu kumuonyesha mpenzi wake wa zamani kuwa hata kama yeye amemwamcha yupo aliempenda zaidi, watu husema mapenzi huongea yenyewe, kama unataka kumkomesha basi tafuta njia nyingine lakini sio ya kukimbilia ndoa ukidhani ataumia, maana huwezi jua na wewe labda utaenda kuumia zaidi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*