Hii ndo mistari mikali ya Stamina kwa mpenzi wake baada ya pete ya uchumba

Baada ya siku ya jana rapper Stamina kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake wa siku nyingi, Veronica, amefunguka mambo machache.

Stamina ameeleza changamoto za mahusiano yao kwa ufupi. Kupitia ukursa wake wa mtandao wa Instagram Stamina ameandika;

Safari yetu ilianzia mbali sana mpaka hapa tulipofikia,,na bado tunaenda mbali mbali zaidi ya tulikotoka,,umenivumilia mengi sana,,vikwazo na matatizo hapa kati tumepitia mengi sana ila bado tukasimama pamoja,,MUNGU ABARIKI KILA HATUA YETU KATIKA MAISHA YETU,,wanga hawakosekanagi katika hili swala ila wamechelewa maana tuna protein za kutoshaa.

Pia Stamina amewashukuru mashabiki wake na watu wake wa karibu kama Roma na mkewe, Nancy kwa kueleza wanamchango mkubwa katika hatua hiyo aliyofikia.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*