UTAFITI: Unywaji Chai ya Moto unaweza sababisha kupata ugonjwa huu

Leo February 24, 2018 nakusogezea utafiti wa Wanasayansi nchini China ambao wamefanya utafiti na kugundua kuwa unywaji wa chai ya moto mara kwa mara unaweza kusababisha kupata saratani ya koo.

Kwa mujibu wa makala iliyochapishwa katika jarida la Annals of Medicine Internal, hali ya afya na tabia ya kula ya watu 456,155 wenye umri kati ya miaka 30-79 ilichunguzwa wakati wa utafiti huo.

Utafiti umefanywa ndani ya miaka kumi na imebainika kuwa watu amabo wanakunywa mara kwa mara chai ya moto au gramu 15 za pombe wana uwezekano mkubwa zaidi wa kupata saratani ya koo, mara tano zaidi ya asiyekunywa.

Na kwa wavuta sigara, kuna uwezekano wa wao kupata ugonjwa huo mara mbili ya mtu asiyevuta sigara.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*