AFYA: Fahamu faida za unywaji maziwa kwa binadamu

Maziwa ni moja ya kimiminika kinachotajwa na kuaminiwa kuwa kinamkinga binadamu na baadhi ya magonjwa pia maziwa ni dawa tosha kwa magonjwa mbalimbali.

Zifatazo ni faida za unywaji maziwa:

i.) Huimarisha meno
Maziwa ni chanzo bora cha madini ya kalisiamu, hivyo basi maziwa ndicho kitu halisi kinachohitajiwa na meno yetu. Pia maziwa huzuia kutoboka na kuoza kwa meno. Kalisiamu hufyonzwa na miili yetu kukiwa na vitamini D;

ii.)Maziwa husaidia kupunguza uzito wa mwili

Utafiti unaonesha kuwa wanawake wanaokunywa maziwa hupunguza uzito zaidi kuliko wale wasiokunywa. Inashuriwa kunywa maziwa wakati wa chakula cha jioni au unapokula matunda.

iii.)Kujenga misuli ya mwili

Hili ni kutokana na protini zinazopatikana katika maziwa. Wanariadha wengi hunywa maziwa baada ya mazoezi, hii ni kwa ajili ya kuupa mwili virutubisho vya kutosha kwa ajili ya kujijenga tena

iv.) Husaidia kupunguza maumivu ya hedhi

Wanawake wengi wanakabiliwa na maumivu wakati wa hedhi. Maziwa yamedhibitishwa kuzuia na kupunguza maumivu haya kwa kiasi kikubwa.

v.) Hupambana na maradhi mengine

Kwa miongo kadhaa tafiti zimebaini kuwa maziwa huzuia magongwa kadha wa kadha. Magonjwa hayo ni kama vile shinikizo la damu na kiharusi. Inaaminika pia maziwa hupunguza lehemu (cholesterol) mwilini na kuongeza uwezo wa macho kuona. Baadhi ya watafiti wameeleza kuwa unywaji wa maziwa huzuia ania fulani za saratani.

 

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*