VIDEO: Johari apigana na Chuchu kisa penzi la Ray

Johari amebainisha hayo kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia ukurasa wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia majira ya saa 8:00 mchana hadi 10:00 alasiri.

“Sijawahi kugombana na Chuchu na wala msanii yeyote nchini yule tokea nimeanza fani hii ya uigizaji. Mimi siwezi kukaa na kugombana na mtu nipo ‘busy’ na kazi zangu watu wanaongea tu hivyo ila mimi siwezi”, amesema Johari.

Pamoja na hayo, Johari ameendelea kwa kusema “hapana sijawahi kuchukia Chuchu Hans alivyoanza kutoka na Ray, kwanini sasa nichukie ?. Sijawahi kuwa na mahusiano yeyote ya kimapenzi na Ray kwa kifupi mimi naomba niongelee kazi zangu za sanaa na maisha yangu maana mara nyingi huwa sipendelei kuzungumzia maisha ya watu”.

Johari ameendelea kufafanua

“Sijawahi hata siku moja kukaa mbele ‘media’ na kuongelea mahusiano ya mapenzi kwa sababu mimi ni mtoto wa kike na sijaolewa kwa hiyo familia yangu haiwezi kuniruhusu kuongelea hivyo vitu”.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*