Emmanuel Mbasha amlilia Flora

Msanii wa injili ambaye aliwahi kuwa mume wa Flora, Emmanuel Mbasha amefunguka na kumshukuru Flora kwa kumzalia mtoto wa kike mzuri lakini pia ametumia nafasi hiyo kutoa malalamiko yake kubaniwa kuonana na mtoto wake huyo kwa muda wa mwaka wa pili.

Mbasha ametumia mitandao ya kijamii kufikisha kilio chake kwa mzazi mwenzie huyo ambaye sasa ameolewa na Daudi Kusekwa na kumtaka japo kumpa haki yake ya kuonana na mtoto wake huyo ambaye anadai kuwa amemlea toka akiwa mdogo.

“Ulinizalia mtoto mzuri sana kwa hilo nakushukuru mno. Nimemmiss Lizy sana unipe basi mtoto unaninyima kabisa daah karibu mwaka wa 2 inaelekea 3 sasa sijamwona mtoto du mimi baba yake tu ila nakuomba hata siku moja moja nifurahie maisha na dogo basi nakuomba nimwone mwanangu Lizy. Najua hata mtoto amenimiss sana mana ameondoka kwangu akiwa mkubwa na nimemlea tangu mtoto ila anashindwa kuongea tu ila najua ananikumbuka sana”

Mbasha aliendelea kumwaga hisia zake juu ya kubaniwa japo kumuona mtoto wake na kusema kuwa anachofanya Flora ni kwenda kinyume na sheria na kupingana na amri ya makama ambayo ilimpa nafasi kama mzazi kumuona mtoto wake.

“Mahakama iliamua mtoto akae na Mama ila niwe namwona mtoto, sasa unapingana na Mahakama. Sitaki povu nimeongea na mzazi mwenzangu X wife, mke wa mtu..njia za kawaida naona imeshindikana unakaza sana aise sasa inabidi nikuombe Insta tu” alisema Mbasha

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*