Tunda amuomba msamaha Aunty Ezekiel

Miezi kadhaa iliyopita kupitia mtandao wa instagram wa video vixen maarufu Tunda alirushiana maneno na muigizaji Aunty Ezekiel pamoja na mzazi mwenzake Mose Iyobo na kusemekana kuwa Tunda alishindwa kulipa deni alilokuwa akidaiwa na Aunty Ezekiel.

Leo March 10,2018 kupitia mtandao wa instagram wa Tunda ameomba radhi kwa kile ambacho alikifanya dhidi ya Aunty na kuamini kuwa hata yeye atakuwa mama wa baadae, hivyo ameamua kuomba radhi.

“Let me take this opportunity kumuomba radhi Aunty kwa kumtukana mtoto wake ilikuwa ni hasira naomba msamaha kama mwanamke ambaye nitaitwa mama pia soon” Ujumbe huo pia umezua maswali kuwa Tunda ni mjamzito? kwa nini asema atakuwa mama soon?.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*