Baada ya Raisi kutoa oyo juu ya maandamano mange kimambi aandika haya

Anaandika mange kimambi

Naombeni mniambie cha kufanya, kuna 2 major international Television networks (Top of the top) na one major international radio network (Vituo viwili vya television vya kimataifa (vikubwa haswa) na kituo kimoja cha radio cha kimataifa)zinaniomba interview kuhusiana na maandamano mpaka sasa nawapiga chenga….
Nawapiga chenga kwa sabbau hizi

1. Naona nikianza kufanya na interview nitaharibu userious wa maandamano itakuwa kama natafuta kiki tu, yani ntawapa wapuuzi cha kusema….
2. I feel like this is not my story to tell, mwisho wa siku mimi nna type tu kwenye simu wanaojirisk ni watu wengine. I don’t deserve this kind of attention. Kutoa idea hata mtoto wa miaka 10 angetoa tu….. I don’t want this to be about me. Kama wanataka kujua si waje TZ wawahoji watu mitaani, tena ndo itapendeza zaidi na kuleta msisimko zaidi
3. Naweza kuulizwa maswali ya kutegwa nkaharibu kama Lowassa na BBC kipindi cha kampeni alivyobanwa mpaka akakosa majibu, alafu hizo clip zikaanza kutumika kuwa discourage waandamanaji.
4: Nna kigugumizi kibaya especially kwenye issue kama hizo za interview na maTV makubwa kama hayo lazma ntakuwa nervous na nikishakuwa nervous au na uwoga au hasira basi kigugumizi ni balaaaa jamani ntagugumia ka bubu! Haki I will come across as a complete fool ??
Pls niambieni nifanyeje? Naombeni nyinyi ndo muamue. Mimi naona nisifanye interview yoyote ile mpaka maandamano yafanikiwe. I think it’s too risky!!!

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*