#Fahamu kitu Wasichotaka kusikia Babu Seya na mwanaye

Wasanii Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha wamefunguka na kuweka wazi kuwa katika maisha yao ya muziki na sanaa hawataki kusikia kitu kinaitwa siasa na kusema wao siyo wanasiasa bali ni wasanii wa muziki.

Babu Seya na mwanaye Papii Kocha wamesema hayo baada ya kusikia tetesi za watu wakiwahusisha na masuala ya siasa na vyama vya siasa na kudai kuwa wao si wanasiasa bali wao ni wasanii wa muziki.

“Hatupo kisiasa sisi bali sisi ni wanamuziki basi hatuna zaidia ya hilo, hata hapa tukiongea tuongee kuhusu muziki ukiniambia hapa niimbe nitaimba ila ukiniambia nikahubiri siasa mimi siwezi sababu si mwanasiasa” alisema Papii Kocha

January 12, 2018 katika mkesha wa miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika viwanja vya Maisara Unguja Babu Seya na mwanaye Papii Kocha walipanda jukwaani kwa mara ya kwanza toka watoke jela katika mkesha huo, jambo ambalo lilifanya baadhi ya watu kuhisi kuwa wanamuziki hao wanatumika na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitu ambacho wao wamekikana na kusema hawahusiki na siasa.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*