Uzalendo wamshinda bosi wa timu, aingia uwanjani na bastola

Mmiliki wa klabu ya PAOK inayoshiriki ligi kuu nchini Ugiriki (Greek Super League), Ivan Savvidis amejikuta akishindwa na uvumilivu na kuingia uwanjani na bastola huku akimuambia mwamuzi umekwisha baada ya kuchelewa kuamuru bao lao lililopatikana katika mchezo wao dhidi ya timu ya AEK .

Katika mchezo huo uliyopigwa jana siku ya Jumapili mchezaji wa PAOK, Fernando Varela aliipatia bao timu yake dakika za mwisho kwa jitihada binafsi kisha mwamuzi akachelewa kuamuru kuwa goli hali iliyopelekea mmiliki wa timu hiyo, Ivan Savvidis kupandwa na jazba na kuingia uwanjani huku akiwa na bastola kiunoni.

Mara baada ya kutokea kwa tukio hilo meneja wa klabu ya AEK, Mhispania, Manolo Jimenez amesema kuwa hawakufahamu kuwa alikuwa na bastola ni ghafla tu wameiyona akiwa nayo na kumuambia mwamuzi umekwisha.

Msimamo wa ligi kuu ya Ugiriki huku PAOK wakishika nafasi ya tatu na alama zao 50 wakati ya kwanza ikishikwa na hasimu wake huyo AEK mwenye pointi 55.

 

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*