Diamond amtaja mrembo aliyewahi kumtoa machozi, adai alikuwa kama yupo peponi

Mapenzi ni matamu kuzidi asali, lakini ukitendwa huwa machungu zaidi ya shubiri. Diamond Platnumz amemtaja mrembo ambaye amewahi kumtoa chozi wakat wapo kwenye mahusiano.

Hitmaker huyo wa African Beauty, amemtaja mrembo huyo ni malkia wa filamu nchini Wema Sepetu.

Akiongea kwenye kipindi cha Msetoea cha Radio Citizen, Diamond amesema, “Enzi za mahusiano yangu na Wema, ameshawahi kuniliza sana.”

Bosi huyo wa WCB pia ameongeza kuwa Babu Tale aliwahi kumwambia ajiweke pembeni kwenye mahusiano hayo wakati yupo na Wema kutokana na penzi hilo kutokuwa sawa, hata hivyo yeye alimjibu kuwa akiwa na mrembo huyo ni kama yupo peponi.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*