Mambosasa Athibitisha Kumkamata Diamond, Kupandishwa Kizimbani – Video

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amethibitisha kukamatwa kwa mwanamuziki, Diamond Platnumz na Nandy kufuatia agizo la Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe, ambaye aliliagiza Jeshi hilo kuwasaka, kuwatia mbaroni na kuwahoji kutokana na tuhuma za kufanya uhuni ndani ya mitandao kwa kusambaza video za utupu.

Kamanda Mambosasa amesema Diamond amekamatwa kwa tuhuma za kupiga picha za utupu na kuzisambaza mitandaoni, amesema taratibu zote za kipolisi bila kujali umaarufu wake na tayari ameshahojiwa na kuachiwa kwa dhamana, wanasubiri kumfikisha mahakamani.

Waziri Mwakyembe alitoa agizo hilo leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) aliyehoji akitaka kujua serikali ina mkakati gani kutokana na wimbi la wasanii kuachia video na picha zao utupu mitandaoni.

Aidha, Mwakyembe alisema Tanzania siyo kokoro la uchafu na kueleza kwamba wanaangalia taratibu za kuwafikisha Diamond na Nandy mahakamani kutokana na tuhuma hizo.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*