Mke wa aliyekuwa Rais wa Marekani Bush amefariki

Barbara Bush, mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani na mwanaharakati amefariki akiwa na umri wa miaka 92.

Barbara alikuwa nguzo ya kisiasa ya marais wawili wa taifa hilo mumewe George HW Bush na mtoto wake George W Bush.

Alikuwa mke wa rais kutoka 1989 hadi 1993 afya yake imekuwa ikiyumba kwa muda sasa na alikuwa amekataa kupatiwa matibabu zaidi.

Mumewe aliye na umri wa miaka 93 ndiye rais aliyeishi kwa muda mrefu nchini Marekani.

Mtoto wao George alichaguliwa 2000 na kukaa madarakani kwa mihula miwili kama rais wa 43 wa Marekani.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*